Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC: Raia wengi wahama makazi yao baada ya mauaji ya hivi karibuni Ituri

Baada ya mashambulizi ya wikendi iliyopita dhidi ya maeneo ya watu waliokimbia makazi yao ya Tshe na Drodro katika mkoa wa Ituri, mashariki kaskazini mwa DRC, hali ya kibinadamu inazidi kuzorota katika eneo hilo.

Kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Bunia, Ituri, mnamo 2018.
Kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Bunia, Ituri, mnamo 2018. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kwa kuhofia maisha yao, wamepokelewa katika kituo cha muda cha tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO,  katika mji wa Roe, ambacho tayari kinawapa hifadhi zaidi ya watu 20,000 waliokimbia makazi. Hata hivyo watu hao wanakabiliwa na uhaba chakula na pesa za kukidhi mahitaji yao ya msingi.

Zaidi ya watu 50,000 waliokimbia makazi yao wamewasili Roe, kulingana na takwimu kutoka Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA).

Watu hawa ambao wana shida nyingi wamekuwa wakilala nje usiku kwa siku tatu mfululizo na pia wanakabiliwa na hali mbaya ya ya kimazingira.

"Tupo hapa na watoto na wazee. Tumechoka na tuna njaa. Tunachoomba kama kipaumbele ni msaada wa chakula, "mwakilishi wa watu hawa waliokimbia makazi yao ameiambia RFI.

Baadhi wanatamani kurejea katika vijiji vyao vya asili lakini hawawezi kwa sababu ya hali mbaya ya usalama katika eneo hilo.

Walinda amani wa MONUSCO, ambao walitumwa huko Drodro, eneo la shambulio, walirudi Roe ili kuimarisha usalama karibu na eneo wanakopewa hifadhi wakimbizi hao wa ndani.

Mazingira ya usalama yanazuia angalau mahirika kumi na saba  kutoa msaada wa kibinadamu, hali ambayo imeathiri watu 300,000 waliokuwa wakihitaji msaada wa dharura huko Drodro, Fataki, Nizi, Lita, Bambu na Mangala.

Zaidi ya watu milioni 1.7 wamehamiakatika mji mùkuu wa mkoa wa Ituri, zaidi ya theluthi moja yao wamekimbilia katika eneo la Djugu, kulingana na OCHA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.