Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Ituri: Magari 1,000 yakwama Komanda kwa kukosa kusindikizwa na jeshi

Kwa zaidi ya wiki moja, takriban magari elfu moja yamekwama huko Komanda, kilomita 75 kusini mwa Bunia katika eneo la Irumu, baada ya jeshi kusitisha zoezi la kusindikiza magari ka ajili ya usalama, kulingana na Radio Okapi.

Bunia, mji mkuu wa Ituri.
Bunia, mji mkuu wa Ituri. HokieRNB/CC/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa shirika la uchukuzi katika mkoa wa Ituri, Georges Bosman, anasema ni vigumu kwao kuingia kwenye barabara ya Komanda-Luna, ambayo ina urefu wa takriban kilomita 65 bila kusindikizwa na jeshi.

Hali ya usalama inayovurugwa na "mashambulizi ya ADF" kwenye barabara hii hairuhusu madereva kuchukua hatari ya kwenda huko.

Wakati wa mkutano wao na Mkuu wa majeshi ya FARDC, Jenerali Mbala Musese, Jumatatu, Novemba 1 huko Bunia, wachukuzi waliomba ushiriki wake kwa "kurejesha zoezi lakusiikiza magari ya raia" na "kurejeshwa kwa usalama" kwenye barabara yenye umuhimu mkubwa kwa uchumi wa mkoa huo.

Jenerali Mbala Musese aliwaahidi kushughulikia suala hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.