Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Guinea: Mohamed Béavogui ateuliwa kuwa Waziri Mkuu

Mfanyakazi mwandamizi wa kimataifa Mohamed Béavogui, ameteuliwa kuongoza serikali ya mpito, ambayo muda wake bado haujabainishwa na utawala wa kijeshi. Béavogui, mwenye umri wa miaka 68, ambaye sio maarufu sana kwa raia wa Guinea, ni mzowefu na mtaalamu katika masuala ya maendeleo.

Mohamed Béavogui, afisa mwandamizi wa umma, ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Guinea kuongoza serikali ya mpito iliyotangazwa na Kanali Doumbouya.
Mohamed Béavogui, afisa mwandamizi wa umma, ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Guinea kuongoza serikali ya mpito iliyotangazwa na Kanali Doumbouya. © Wikimédia / Travail personnel - Lagabara 07
Matangazo ya kibiashara

Katika agizo lililokuwa linasubiriwa kwa siku kadhaa, ambalo lilisomwa kwenye runinga ya taifa, mkuu wa utawala wa kijeshi, Kanali Doumbouya, amemteua mkongwe wa maendeleo kwa wadhifa wa Waziri Mkuu. Mohamed Béavogui, ambaye ameteuliwa kwa wadhifa huu, ana uzoefu wa miaka zaidi ya 30 akihudumu katika mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.

Alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya usimamizi wa majanga katika Jumuiya ya Mutual Pan-African huko New York kabla ya kushika nyadhifa zingine ndani ya Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), na FAO, mfuko wa Shirika la Chakula na Kilimo huko Roma, Italia.

Mbali na siasa za ndani

Kiongozi mpya wa serikali ya Guinea atakuwa na jukumu la kutekeleza hati ya mpito iliyoandaliwa siku chache baada ya jeshi kuchukua madaraka. Hati hii inabainisha katika Ibara ya 51, pamoja na mambo mengine, kwamba Waziri Mkuu anaongoza, anaratibu na kuhuisha hatua za serikali.

Kwa kumteua Waziri Mkuu asiye na uzoefu wa kiserikali, Kanali Doumbouya alichagua mtu aliye mbali na siasa za ndani na ambaye hashukiwi kushiriki katika mgogoro wa ndani wa miaka ya hivi karibuni.

Mohamed Béavogui alikuwa aliombwa kushikilia wadhifa huu wakati wa utawala wa hayati Jenerali Lansana Conté mnamo mwaka 1987, siku moja baada ya vurugu za kijamii na migomo ya mara kwa mara ambayo ilitikisa utawala wa wakati huo na kumlazimu rais wa zamani kumteua Lansana Kouyaté kushikilia wadhifa huo.

Mbali na lugha kadhaa zinazozungumzwa nchini Guinea, Mohamed Béavogui pia anazungumza Kifaransa, Kiingereza, Kirusi na Kiitaliano. Alizaliwa Agosti 15, 1953 huko Porédaka katikati mwa Guinea, ana mke na ni baba wa watoto 4.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.