Pata taarifa kuu

Malaria: WHO yaagiza kupelekwa kwa chanjo ya RTS, S kwa watoto

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeagiza kupelekwa kwa chanjo ya Malaria kwa watoto wanaoishi Kusini mwa Jangwa la Sahara na katika maeneo yaliyo hatarini.

Ghana ni moja ya nchi tatu katika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zilianza kutumia chanjo ya Malaria katika mikoa iliyochaguliwa tangu mwaka 2019.
Ghana ni moja ya nchi tatu katika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo zilianza kutumia chanjo ya Malaria katika mikoa iliyochaguliwa tangu mwaka 2019. AFP - CRISTINA ALDEHUELA
Matangazo ya kibiashara

Daktari Tedros Adhanom Ghebreyesus amezungumzia kuhusu "wakati wa kihistoria". "Chanjo ya malaria inayosubiriwa kwa muda mrefu kwa watoto ni mafanikio ya sayansi, afya ya watoto na mapambano dhidi ya Malaria," mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani amesema katika taarifa. Amebaini kwamba, matumizi ya chanjo hii pamoja na zana zilizopo za kuzuia malaria inaweza kuokoa "makumi ya maelfu ya maisha ya vijana kila mwaka".

RTS, S ni chanjo inayofanya kazi dhidi ya vimelea vinavyoambukizwa na mbu (Plasmodium falciparum), vimelea hatari zaidi ulimwenguni na vilivyoenea zaidi barani Afrika.

Kwa upande wa Afrika, ambapo Malaria inaua zaidi ya watoto 260,000 walio chini ya umri wa miaka mitano kila mwaka, chanjo hii ni sawa na matumaini, hasa wakati hofu ya kujidhatiti kwa malaria kwa matibabu inaongezeka. "Kwa karne nyingi, malaria imeshambulia ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, na kusababisha mateso makubwa," amesema Dk Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO katika kanda ya Afrika. "Tumetarajia kwa muda mrefu kupata chanjo ya Malaria inayofaa na sasa, kwa mara ya kwanza, tuna chanjo iliyopendekezwa kwa matumizi mengi," ameongeza.

Tangu mwaka wa 2019, nchi tatu za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ghana, Kenya na Malawi, zilianza kutumia chanjo hiyo katika maeneo yaliyochaguliwa ambapo maambukizi ya malaria yamekuwa yakiongezeka. Miaka miwili baada ya kuanza kwa kipimo hiki cha kwanza cha ukubwa ulimwenguni, dozi milioni 2.3 ya chanjo iliweza kutolewa.

Chanjo nyingine iliyotengenezwa na watafiti katika Chuo Kikuu cha Oxford na Burkina Faso imeonekana kuwa na ufanisi wa 77% katika majaribio ya awamu ya 2. Awamu ya 3 itakamilika katika miaka miwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.