Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Guterres aumizwa na hatua ya Ethiopia ya kuwafukuza wanadiplomasia saba wa UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio  ameelezea kwa taarifa wasiwasi wake baada ya Ethiopia kutangaza kuwatimua wakuu saba wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema Umoja wa Mataifa unatoa misaada ya kuokoa maisha ya watu nchini Ethiopia.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema Umoja wa Mataifa unatoa misaada ya kuokoa maisha ya watu nchini Ethiopia. John Minchillo POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Shughuli zote za kibinadamu za Umoja wa Mataifa zinaongozwa na kanuni za kimsingi za binadamu, kutopendelea, na kwa uhuru", amesema António Guterres, abaini kwamba "ameshtushwa" na uamuzi huo.

"Nchini Ethiopia, Umoja wa Mataifa unatoa misaada ya kuokoa maisha ya watu- ikiwa ni pamoja na chakula, dawa, maji na vifaa vya usafi - kwa wale wenye mahityaji makubwa, " amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kubaini kwamba ana "imani kamili kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambao wako nchini Ethiopia kufanya kazi hii".

Hatua hii ya Ethiopia inakuja baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kuwa, watu katika jimbo lenye mzozo la Tigray nchini Ethiopia, wanaendelea kukabiliwa na baa la njaa na hali inaendelea kuwa mbaya kutokana na ukame unaoshuhudiwa.

Wiki hii Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na misaada ya kibinadamu Martin Griffiths alisema hali ni mbaya sana na watu katika jimbo la Tigray, wanakula mizizi ya mimea na maua kwa sababu hawana chakula. Griffiths alisema hali hii inaleta kumbukumbu ya hali ya ukame iiyoshuhudiwa nchini humo miaka ya 80 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya Milioni moja kwa kukosa chakula.

Ethiopia yakanusha madai dhidi yake

Aidha, Mkuu huyo wa Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa, aliishtumu serikali ya Ethiopia kwa kuzuia vyakula na dawa kuwafikia watu katika jimbo hilo, ambalo mpaka sasa asilimia 22 ya watu wanakabiliwa na utapiamlo.

Hata hivyo, serikali ya Ethiopia imeendelea kukanusha kuwa, inazuia magari yanayobeba misaada ya kibinadamu kuwafikia walengwa wakati huu maelfu ya watu wakiendelea kuteseka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.