Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA

Sudan: Mvutano wapungua baada ya makubaliano kati ya mamlaka na waandamanaji

Shughuli ya usafirishaji wa mafuta kutoka Sudan Kusini, iliyozuiwa tangu Jumamosi, inatarajia tena kuanza . Makubaliano yalifikiwa Jumapili jioni, Septemba 26, 2021, baada ya mkutano kati ya waandamanaji na ujumbe wa maafisa kutoka Khartoum.

Vikosi vya usalama vilitumwa huko Port Sudan.
Vikosi vya usalama vilitumwa huko Port Sudan. ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bandari ya jiji, kwa upande mwingine, bado imefungwa, kama vile barabara inayounganisha mji wa Port Sudan na mji mkuu, barabara kuu ya nchi hiyo.

Kuzuiwa kwa barabara hiyo inayoelekea katika mji wa Port Sudan kumekuwa kukiendelea kwa siku kumi, lakini wikendi hii mvutano ulikuwa umeongezeka sana. Baada ya bandari na uwanja wa ndege, waandamanaji walishambulia vituo vya mafuta vya mji huo. Walifunga mabomba mawili, pamoja na lile la Bashayer, bomba pekee linalotumiwa na Sudan Kusini kuleta mafuta yake nchini Sudan na nchini humo husafirishwa hadi kwenye masoko ya kimataifa.

Bomba hilo ni la kimkakati lenye uhusiano kati ya nchi hizo mbili, lakini pia kwa Khartoum. Mwishoni mwa wiki hii iliyopita Wizara ya mafuta ya Sudan ilionya kuwa ina siku kumi tu za akiba ya haidrokaboni. Kutokana na uzito wa hali hiyo, ujumbe wa ngazi ya juu  ulikwenda katika mji wa Port Sudan siku ya Jumapili, ukiongozwa na Jenerali Kabashi, mjumbe mwenye ushawishi wa Baraza kuu la utawala, taasisi inayoundwa na wanajeshi na raia ambayo inasimamia serikali ya mpito. Mawaziri wa Mambo ya nje, Mambo ya Ndani, Nishati na Uchukuzi pia walikuwa katika ujumbe huo.

Wamehakikishiwa kuondolewa kwa zuio la bomba la mafuta na uwanja wa ndege wa jiji, lakini bandari bado iko chini ya waandamanaji ambao wanalaani makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwaka jana kati ya Khartoum na makundi mbalimbali ya waasi na ambao wanabaini wamedhulumiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.