Pata taarifa kuu
GUINEA

Guinea: Wafungwa wa kisiasa kuachiliwa hivi karibuni

Viongozi wa mapinduzi nchini Guinea wameahidi kufanya kilio chini ya uwezo wao kuachiliwa haraka wanasiasa na wafuasi wa upinzani waliokamatwa chini ya utawala wa rais aliyeondolewa madarakani Alpha Condé, ambao wanaendelea kusubiriwa kwa hamu na ndugu na jamaa zao.

Raia wakishangilia wanajeshi baada ya ghasia zilizosababisha kupinduliwa kwa Rais Alpha Condé katika kitongoji cha Kaloum, huko Conakry, Guinea Septemba 6, 2021.
Raia wakishangilia wanajeshi baada ya ghasia zilizosababisha kupinduliwa kwa Rais Alpha Condé katika kitongoji cha Kaloum, huko Conakry, Guinea Septemba 6, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi pia wamebaini tena katika taarifa zao za hivi karibuni, zilizosomwa kwenye runinga ya taifa na kurushwa kwenye mitandao ya kijamii, kuanzishwa kwa  "mashauriano" ya kitaifa kufafanua utaratibu wa kipindi cha mpito katika nchi hii masikini ya Afrika ya Magharibi.

Serikali ijayo ya "umoja wa kitaifa" itakuwa na kazi ya kuongoza kipindi hiki cha mpito, kiongozi mkuu wa mapinduzi Luteni-Kanali Mamady Doumbouya, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter leo Jumanne.

Luteni-Kanali Doumbouya pia ameiagiza "Wizara ya Sheria leo (Jumatatu) kuwasiliana na ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu, mamlaka ya magereza na wanasheria ili kufanya uchambuzi wa kina wa faili ya wafungwa wa kisiasa ili waachiliwe mapema iwezekanavyo ", kulingana na taarifa iliyosomwa katika taarifa ya habari ya televisheni Jumatatu jioni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.