Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Afrika Kusini: Watu saba wakamatwa kwa mauaji ya afisa wa serikali

Polisi wa Afrika Kusini inachunguza mauaji ya Babita Deokaran, afisa wa serikali katika mkoa wa Gauteng, ambayo ni pamoja na Johannesburg. Alifichua ufisadi unaozunguka mikataba ya umma ya udanganyifu kuhusiana na Covid-19, kwa niaba ya "Covidpreneurs", wajasiriamali hawa ambao wamejitajirisha kinyume cha sheria kutokana na janga hilo.

Babita Deokaran, aliyeuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake Jumatatu, alikuwa mmoja wa mashahidi muhimu katika Kitengo Maalum cha Upelelezi cha Polisi ya Afrika Kusini.
Babita Deokaran, aliyeuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake Jumatatu, alikuwa mmoja wa mashahidi muhimu katika Kitengo Maalum cha Upelelezi cha Polisi ya Afrika Kusini. AFP/STEPHANE DE SAKUTIN
Matangazo ya kibiashara

Watu saba walikamatwa Ijumaa, Agosti 27, 2021. Uchunguzi unaendelea kujua ikiwa kifo chake kinahusishwa na msimamo wake dhidi ya ufisadi.

Babita Deokaran alipigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yake Jumatatu baada ya kumfikisha binti yake shuleni.

Ikiwa polisi bado hawajaonyesha sababu zinazohusiana na mauaji hayo, mkuu wa mkoa wa Gauteng David Makhura amebaini wazi kwamba kifo hicho kinahusiana na kesi za ufisadi zinazoathiri utawala wa mkoa huo.

Afisa huyo mwenye umri wa miaka 53, aliye kuwa anasimamia idara ya afya ya mkoa kabla ya kifo chake, alikuwa shahidi muhimu katika kitengo cha uchunguzi maalum cha polisi, katika kesi ya mikataba ya umma inayohusishwa na udanganyifu.

Kulingana na kitengo hiki, mikataba hiyo, iliyochafuliwa na ulaghai au malipo zaidi, imegharimu karibu euro milioni 20 za matumizi yaliyotolewa ili kupatia mkoa vifaa vya kinga dhidi ya Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.