Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Wakazi wa Tigray wakabiliwa na uhaba wa chakula

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kwa mara nyingine ametoa wito wa usitishwaji wa vita katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, eneo ambalo wanajeshi wa serikali wamekuwa wakipambana na waasi wa jimbo hilo.

Kwa upande wake Marekani imetahadharisha kuwa msaada wa chakula utaisha wiki hii kwa mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa katika eneo la Tigray nchini Ethiopia.
Kwa upande wake Marekani imetahadharisha kuwa msaada wa chakula utaisha wiki hii kwa mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa katika eneo la Tigray nchini Ethiopia. REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hali ya kibinadamu ni mbaya Ethiopia na kuzitolea wito pande zinazopigana zisitishe mapigano mara moja.

” Wananchi wa Ethiopia wameteseka sana.Β Mazingira ya hali ya kibinadamu ni mabaya sana. Mamilioni ya watu wanahitaji msaada. Miundo mbinu imeharibiwa, na tumepata ripoti kuwa wanawake wamedhulumiwa sana, na kuendelea kwa machafuko kunaendelea kufanya mambo kuwa mabaya zaidi”, amesema Antonio Guterres.

Nalo Shirika la Marekani linalohusika na utoaji wa misaada ya kibinadamu, linaonya kuwa mamilioni ya watu wapo katika hatari ya kukosa chakula kwa sababu ya uhaba wa vyakula mbalimbali.

Kwa upande wake Marekani imetahadharisha kuwa msaada wa chakula utaisha wiki hii kwa mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa katika eneo la Tigray nchini Ethiopia. Siku ya Alhamisi mkuu wa shirika la misaada la Marekani, USAID, Samantha Power, alisema katika taarifa kwamba chini ya asilimia saba ya chakula kinachohitajika kimekuwa kikifika eneo la Tigray lenye wakaazi milioni sita na USAID na mashirika mengine yameshatumia hazina yote ya chakula kilichokuwa kikihifadhiwa katika maghala ya Tigray baada ya miezi tisa ya vita.Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.