Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-AFYA

Cote d'Ivoire: Mpango wa kudhibiti ugonjwa wa Ebola uko tayari kuwekwa

Tangu kutangazwa Jumamosi Agosti 14 kesi moja ya ugonjwa wa virusi vya Ebola, idara za afya na wale wanaohusika na magonjwa ya milipuko wako tayari kujaribu kudhibiti maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo. Mapambano yanaendelea.

Mhudumu wa afya atoa chanjo ya Ebola huko Gueckedou, Guinea,  Februari 23, 2021 (Picha ya kumbukumbu).
Mhudumu wa afya atoa chanjo ya Ebola huko Gueckedou, Guinea, Februari 23, 2021 (Picha ya kumbukumbu). © RFI / Carol Valade
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili, wizara ya afya kwa ushirikiano na washirika wake kama shirika la afya Duniani (WHO), Benki ya Dunia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF), shirika la Msalaba Mwekundu imetoa mpango wa kinga na mpango mwingine. Madawa hayo yatasambazwa kuanzia Jumanne kote nchini.

Mpango una vipengele viwili, kinga na majibu. Kijana wa miaka 18 ambaye alipatikana na virusi vya Ebola ametengwa na anahudumiwa katika Hospitali  ya CHU huko Treichville. Jumapili Agosti 15, chanjo 5,000 za kupambana na Ebola zilifika katika mji wa Abidjan kutoka nchini Guinea, ameripoti mwandishi wetu huko Abidjan, Jean-Luc Aplogan.

"Watu wanaolengwa kupewa chanjo hiyo", ni wahudumu wa afya, vikosi vya usalama katika maeneo ya mipaka, ambapo mgonjwa alipita na wale ambao walisafiri naye, watapewa chanjo. Safari ya mgonjwa huyo ilianza nchini Guinea na kuishia Abidjan na alitumia basi lililokuwa na abiria 32.

Guinea yashindwa kuipata familia ya mgonjwa

Kwa upande wa Guinea, bado kazi ni mgumu kwani mamlaka husika zimeshindwa kuipata familia ya msichana huyo, kulingana na mwandishi wetu huko Conakry, Mouctar Bah. Kulingana na vyanzo vya hospitali nchini Guinea, simu zao zimezimwa.

Dk Sakoba Kéita, mkurugenzi wa mamlaka ya Usalama wa Afya nchini Guinea anasema: "kipaumbele cha kwanza ni kuchanja watu wote waliotengamana na mgonjwa ndani ya kipindi cha saa 48 baada ya kugunduliwa kwa virusi hivyo. Kwa hivyo Guinea itatoa dozi 5,000 za chanjo kwa Côte d'Ivoire na kutuma timu ya wajumbe 5 ili chanjo hiyo ianze leo ".

WHO na UNICEF kwa upande wao wako tayari kutoa huduma zinazohitajika kwa haraka kwa mgonjwa aliyepatikana na virusi vya Ebola, amesema Georges Alfred Ki-Zerbo, mwakilishi wa WHO nchini Guinea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.