Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa yasitisha makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Ethiopia

Hali ya usalama inazidi kuwa mbaya Kaskazini mwa Ethiopia. Mkataba huo ulianza mnamo mwaka 2019, wakati Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipozuru Addis Ababa

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed huko Jimma, Ethiopia, Juni 16, 2021.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed huko Jimma, Ethiopia, Juni 16, 2021. Marco Longari AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Miaka miwili iliyopita, kutiwa saini kwa makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi ilikuwa ishara ya uhusiano kati ya Ufaransa na Ethiopia mpya ya Abiy Ahmed. Emmanuel Macron alijipongeza wakati huo "kwa kusaini makubaliano na kiongozi ambaye aliamua kujenga amani katika eneo ya Pembe ya Afrika". Ufaransa ilikuwa ikishiriki katika mafunzo ya jeshi la baadaye la wanamaji la Ethiopia.

Mradi huu sasa umesitishwa, ishara ya kuzorota zaidi kwa uhusiano kati ya Abiy Ahmed na washirika wake wa Magharibi. Mazingira ya kisiasa ya Ethiopia yako mbali na matarajio ya ikulu ya Elysée. Miezi tisa ya vita huko Tigray imesababisha nchi kudorora kiusalama. Serikali ya Abiy Ahmed, aliyewahi kupendwa sana na nchi za Magharibi - Waziri Mkuu aliyeshinda Tuzo ya Amani ya Nobel mnamo 2019, sasa anakabiliwa na tuhuma nyingi za ukiukaji wa haki za binadamu.

Paris imesitisha ushirikiano hadi hapo itakapotangazwa tena. Kulingana na chanzo cha kidiplomasia, hata uhusiano wa uaminifu kati ya nchi hizo mbili umedorora kwani Ethiopia imekuwa ikitoa kauli mbovu na za wazi dhidi ya nchi za Magharibi kwa miezi kadhaa.

Mbali na ushirikiano huu na jeshi la wanamaji la Ethiopia, kwa sasa makubaliano yote ya ulinzi ya 2019 yako mashakani. Ufaransa bado hayajaidhinisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.