Pata taarifa kuu
MUSUMBIJI - USALAMA

Filipe Nyusi : Tutawashinda wanajihadi Cabo Delgado

Rais wa Musumbiji Filepe Nyusi, amesema ana matumaini serikali yake itawadhibiti wanajihadi wanaotatiza usalama kwa kuwaua raia katika mkowa wa Cabo Delgado.

Rais wa Musumbiji Felipe Jacinto Nyusi
Rais wa Musumbiji Felipe Jacinto Nyusi AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Nyusi, akizungumza  wakati wa sherehe za 46 za uhuru wa taifa hilo, amesema wanajeshi wa taifa hilo kwa ushirikiano na wale kutoka nje, karibuni watalimaliza shughuli zote za wanajihadi katika mkowa Cabo Delgado.

Operesheni kali ya kuwasaka na kuwatokomeza wanajihadi hao itaendeshwa hivi karibuni, na usaidizi wa kutosha kutoka kwa  mataifa ya SADC, na mengine yanayojali usalama wetu,’alisema rais Nyusi

Juma lililopita viongozi wa mataifa ya SADC, walikubaliana kuwatuma wanajeshi nchini Musumbiji, kulisaidia taifa hilo kutokemeza wanajihadi.

Katika mkutano huo, rais Nyusi, alitoa wito kwa mashirika ya kiraia kuendelea kusaidia raia wa Cabo Delgado, ambao wamekimbia makwao kutokana na shughuli za wanajihadi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.