Pata taarifa kuu
DUNIA-AFYA

Shirika la WHO lasema mataifa karibu 12 yakumbwa na wimbi la tatu la maambukizi ya Covid-19

Shirika la afya duniani WHO linasema mataifa mengi barani Afrika, yanashuhudia wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya Covid 19, wakati huu pia yakiendelea kushuhudia uhaba wa chanjo, huku hospitali kwenye nchi nyingi zikiripoti kuzidiwa uwezo kutokana na ongezeko la wagonjwa.

Afisa wa WHO akipewa chanjo dhidi ya Covid-19
Afisa wa WHO akipewa chanjo dhidi ya Covid-19 Simon MAINA AFP/File
Matangazo ya kibiashara

WHO inasema hadi sasa mataifa karibu 12 yameripoti ongezeko la wagonjwa na aina mpya ya virusi, wakati huu pia mataifa hayo yakikabiliwa na uhaba wa chanjo.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO barani Afrika, Matshidiso Moeti anaonya kuwa wimbi hili la tatu ni hatari.

Na kwamba linakuja kwa kasi sana, na watu wnegi wanaambukiwa sana kwa sababu linasambaa kwa haraka, tunatarajia kuona ongezeko kubwa ziaid ndnai ya wiki tatu zijazoi, hii ni hatari sana; nah ii inaonesha kuwa tutashuhdiia hali mbaya, janga hili linaongezeka katika mataifa 12 na tunachunguza kwa makini ongezeko katika mataufa mengine 14.

Hadi sasa bara la Afrika limerekodi maambukizi milioni 5 na vifo laki 1 na elfu 39.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.