Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA

Berlin: Mkutano wa pili wa kimataifa juu ya Libya kuimarisha maendeleo ya hivi karibuni

Ujerumani na Umoja wa Mataifa zinawaleta pamoja wawakilishi wa Libya na nchi zenye maslahi katika nchi hiyo kwenye mkutano unaokusudia kujadili masuala kadhaa ikiwemo uchaguzi na kuondolewa kwa mamluki wa kigeni

Sehemu ya jeshi la Uturuki lililopelekwa Libya, kwa msaada wa jeshi la muungano wa kitaifa unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa (GNA).
Sehemu ya jeshi la Uturuki lililopelekwa Libya, kwa msaada wa jeshi la muungano wa kitaifa unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa (GNA). AP - Hazem Ahmed
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo utakaofanyika katika ofisi ya wizara ya mambo ya nje mjini Berlin unatarajiwa kuhudhuriwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken.

Mkutano huo unafuatia ule uliofanyika Januari 2020 ambapo viongozi walikubaliana kuweka chini silaha na kushinikiza pande zinazohasimiana kusitisha kabisa mapigano.

Ujerumani imejaribu kuwa mpatanishi mkuu. Nchi ambazo zimehusika katika mchakato huo ni pamoja na nchi tano wanachama wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Italia, Uturuki na muungano wa Falme za kiarabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.