Pata taarifa kuu
BURUNDI-HAKI ZA BINADAMU

Mashirika 12 ya kimataifa ya haki za binadamu, yasikitika Umoja wa ulaya kuisaidia tena Burundi

Mashirika kumi na mawili ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na HRW, FIDH na hata EurAc, yanaelezea katika barua ya wazi iliyowasilishwa kwa umma Jumatatu, Juni 21, wasiwasi wao kuona Umoja wa Ulaya ukijiandaa kuanza tena kutoa msaada wake wa moja kwa moja kwa serikali ya Burundi.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye.
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye. AFP Photos/Tchandrou Nitanga
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Burundi amesema hapo jana Jumatatuhuko Bujumbura kwamba hatuwa hiyo imepasishwa  katika vikao vya wataalamu wa Umoja wa Ulaya.

Claude Bochu balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Burundi amesema kuna hatuwa chanya zilizopigwa na serikali ya Burundi kuelekea kuondolewa vikwazo. Hata hivyo mashirika yalioandika barua hiyo yanasema licha ya kuachiwa huru kwa waandishi wa bahari wa gazeti la Iwacu pamoja na msamaha wa rais kwa wafungwa 2600, bado ni mapema sana kwani mpaka sasa haki za binadamu nchini Burundi bado ni kikwazo

Gisela Castro, mjumbe wa FIDH kwenye Umoja wa Ulaya huko Brussels, anaelezea tahadhari iliotolewa na mashirika hayo.

Kwamba Pamoja na mabadiliko ya serikali mwaka jana, kwa kweli, tulikuwa na uwazi fulani, lakini hakuna mafanikio madhubuti na hakuna maendeleo madhubuti yaliyofanywa juu ya maswala kadhaa ambayo ni muhimu sana kwa mashirika yetu.

Kaongeza kuwa Umoja wa Ulaya umeanza tena mazungumzo ya kisiasa na Burundi, ambayo ni jambo zuri, lakini inajiandaa kuondoa hatua zote zilizokuwa zimechukuliwa, wakati hakuna mabadiliko makubwa yamezingatiwa.

Inaonekana kwamba Ufaransa iko juu kwa wale wanaoshinikiza kuanza haraka kwa ushirikiano, wakati wengine, kama Ubelgiji, au Uholanzi, wanatarajia kuona hatuwa za kujitolea zaidi kutoka Burundi." amesema Gisela Castro, mjumbe wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu FIDH kwenye Umoja wa Ulaya huko Brussels

Hayo yanajiri wakati mahakama jijini Bujumbura ikitangaza kupunguza kifungo cha miaka 32 jela hadi mwaka mmoja kwa mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Burundi Gervais Rukuki. Hatuwa ambayo imefanyika baada ya balozi wa Umoja wa Ulaya Claude Bochu kukutana na rais wa Burundi Evarsite Ndayishimiye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.