Pata taarifa kuu

Niger yafungua tena mipaka yake baada ya kufungwa kwa miezi 15 kudhibiti Corona

Serikali ya Niger imefungua tena mipaka ya nchi yake baada ya kufungwa kwa miezi 15 ili kukabiliana na maambukizi ya janga la virusi vya Corona.Hatua hii imekuja baada ya mafanikio ya kudhibiti maambukizi hayo na kampeni ya utoaji chanjo.

Rais wa Niger Mohamed Bazoum akiiombea nchi yake baada ya kujinyakulia ushindi wa uchaguzi nchini mwake
Rais wa Niger Mohamed Bazoum akiiombea nchi yake baada ya kujinyakulia ushindi wa uchaguzi nchini mwake Issouf SANOGO AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Moussa Sidi, ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara nchini humo,  anakaribisha uamuzi huu akisema ni hatua ambayo itarahisisha uwepo wa ushirikiano wa wakaazi wa eneo la mpakani baina ya mataifa haya mawili.

Niger, moja ya nchi masikini zaidi ulimwenguni, ilichukua hatua hiyo hivi karibuni ili kuzuia kuenea kwa coronavirus baada ya kesi za kwanza kuibuka mnamo Machi 2020.

Mamlaka iliamuru kufungwa kwa mipaka, kutangazwa kwa hali ya dharura na amri ya kutotoka nje, kufungwa kwa maeneo ya ibada na shule, na kutengwa kwa mji mkuu Niamey katika nchi nzima.

Serikali ya Niger inatarajia kutumia hatua hiyo kuanza tena kuimarisha uchumi wake ulioyumba kutokana na  janga la Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.