Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Wakimbizi kutoka Goma waliokimbilia Sake wakabiliwa hali ngumu

Wiki mbili baada ya mlipuko wa volkano ya Nyiragongo, matetemeko ya ardhi hayasikiki wala kuripotiwa tena katika mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 

Moja ya familia za wakazi mji wa Goma wakitoroka makazi yao, baada ya mlipuko wa volkano ya Nyiragongo, Mei 27, 2021.
Moja ya familia za wakazi mji wa Goma wakitoroka makazi yao, baada ya mlipuko wa volkano ya Nyiragongo, Mei 27, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Wakimbizi hao wamekuwa wakirundi makwao kwa wingi bila kusubiri uamuzi wa mamlaka katika mkoa huo. Lakini wengine ambao wamejikuta nyumba zao ziliiharibiwa bado wako katika eneo la Sake, kilomita 27 kutoka mji wa Goma ... Wanaishi katika mazingira magumu.

Katika Shule ya Msingi ya Fazili, shughuli zimesitishwa tangu Mei 23. Majengo yote yanakaliwa na wakimbizi.

"Naomba serikali yetu isitusahau. Watu wanahitaji msaada hapa. Wengine wanahitaji magongo ya kutembelea, wengine wanahitaji baiskeli. Hapa pia tunakabiliwa na njaa. Tunaomba msaada, " amesema Jean-Jacques, mmoja wa wakimizi hao akihojiwa na mwandishi wetu Patient Ligodi 

Kavira, mkimbizi mengine,  ana watoto tisa. Familia nzima hulala  kwenye hema katika moja ya madarasa, hema ambayo walipewa na shirika moja la kutoa misaada.

"Baba, mama, watoto, tunalala hapa usiku. Hakuna heshima. Hakuna utu. Hatuna blanketi, hatuna nguo za kutosha. Tunateseka na baridi. Unavyoona madirisha haya na milango yake vinabaki wazi. Watoto wameanza kukohoa. Hapa tunaishi katika mazingira magumu kabisa. "

Kulingana na habari iliyoripotiwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya kibinadamu, OCHA, angalau wanawake wajawazito 29 wanaoishi katika kambi katika jijmji wa Sake hawana huduma nzuri za kiafya.

Kwa upande wake, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto na wanawake, UNICEF limeripoti kuongezeka kwa idadi ya visa vya kuhara, na visa viwili vilivyothibitishwa vya Ugonjwa wa Homa ya matumbo au Ugonjwa wa Salmonella (salmonellosis).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.