Pata taarifa kuu
Chad

Chad yatumbukia katika sintofahamu baada ya kifo cha Idriss Déby

Katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena, wengi wana huzuni na wengine wengi wanajiuliza hatima ya taifa hilo, siku moja baada ya kifo cha rais Idriss Deby Itno.

Huko Ndjamena, vifaru vinatumwa karibu na ikulu ya rais, Chad, Aprili 20, 2021.
Huko Ndjamena, vifaru vinatumwa karibu na ikulu ya rais, Chad, Aprili 20, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Idriss Deby Itno, madarakani tangu 1990 alifariki dunia Jumatatu Aprili 19 kutokana na majeraha aliyoyapata alipokuwa akiongoza mapigano dhidi ya waasi wa FACT.

Wakaazi wa mji wa Ndamena wana huzuni na wengi wameingiliwa na wasiwasi.

Idriss Deby Itno aliingia madarakani kwa mtutu wa bunduki na ametoka kwa mtutu wa bunduki.

Rais huyo mwenye miaka 68, ambaye alikuwa amechaguliwa kuliongoza taifa lake kwa muhula wa sita ameuawa vitani na waasi, na kuandikisha ukomo wa mtawala ambaye alisifika kwa uwezo wake vitani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.