Pata taarifa kuu
BENIN

Uchaguzi Benin: Mvutano wazua hofu ya kukatwa kwa mtanda wa intaneti

Mvutano umeongezeka nchini Benin baada ya watu wawili kufariki dunia wakati vikosi vya usalama viliwatawanya waandamanaji kwa kufyatulia risasi za moto katikati mwa nchi.

Siku ya uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2019 huko Benin, mtandao wa intaneti ulikataliwa.
Siku ya uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2019 huko Benin, mtandao wa intaneti ulikataliwa. © RFI/Aurore Lartigue
Matangazo ya kibiashara

Hali hii inayoendelea nchini Benin imefanya watu wengi kuwa na hofu ya kukatwa kwa mtandao wa intaneti. Wakati wa uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2019, mtandao wa itaneti ulikatwa.

"Kwa sasa, intaneti inafanya kazi, lakini tuna wasiwasi kwa siku ya uchaguzi," amesema Eskile, mfanyabiashara katikati mwa mji wa Cotonou, akiwa na simu zake mbili mkononi. "Kuna uvumi ambao unasema kutokana na mgogoro huu, kuna hatari ya kukatwa kwa mtandao wa intaneti ili kuzuia usambazaji wa habari uzushi na uongo kwenye mitandao ya kijamii," Sidi Mohammed, dereva wa pikipiki kukodiwa (ZEM) nchini Benin amesema.

Savè yakabiliwa na hali ya sintofahamu

Huko Savè, wilaya iliyo katikati mwa nchi, Alhamisi ilikuwa katika hali ya wasiwasi: wanajeshi waliingilia kati kuondoa vizuizi kwenye barabara kuu ya Parakou, wakifyatua risasi za moto kwa waandamanaji na kuua wawili.

Idadi ya vifo imeongezeka. Vyanzo vya ndani vinaripoti kifo cha pili huko Savè. Mtu huyo aliyefariki dunia ni mmoja wa waliojeruhiwa, siku ya Alhamisi. Kufikia sasa ripoti zinasema kuwa watu wawili walifariki dunia na wanne waliruhiwa katika eneo hilo. Vyanzo rasmi pia vinaripoti majeraha kwa upande wa jeshi.

Jiji hilo, lililoko kilomita 250 kaskazini mwa Cotonou, sasa linaonekana kama mji unaokabiliwa na machafuko. Watu wamelazimika kusalia manyumbani, hakuna masoko, hakuna burudani. Kuna hali ya watu kutotoka nje. Jeshi bado lipo, linaendelea kukagua barabara ili kuzuia vizuizi zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.