Pata taarifa kuu
MSUMBIJI

Jeshi la Msumbiji ladai kuua idadi ‘kubwa’ ya waasi Palma

Idadi "kubwa" ya waasi wameuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya Msumbiji katika operesheni ya kujaribu kuudhibiti mji wa kaskazini mashariki mwa Palma, ambao ulianguka mikononi mwa makundi ya wanamgambo wa kiislamu baada ya shambulio la umwagaji damu mnamo Machi 24, jeshi limesema.

Wanajeshi wa Msumbiji katika mji wa Cabo Delgado uliovamiwa na wanamgambo wa kiislamu.
Wanajeshi wa Msumbiji katika mji wa Cabo Delgado uliovamiwa na wanamgambo wa kiislamu. ADRIEN BARBIER AFP
Matangazo ya kibiashara

"Bado peresheni haijamalizika (...) lakini idadi kubwa ya magaidi wameuawa kwa katika operesni hiyo," kamanda wa operesheni huko Palma, Chongo Vidigal, amewaambia waandishi wa habari.

Siku kumi na moja zilizopita, makundi yenye silaha yalishambulia mji wa bandari wa kimkakati katika uvamizi ulioandaliwa kwa uangalifu, uliozinduliwa kilomita chache tu kutoka eneo kunakoendeshwa mradi mkubwa wa gesi wa mabilioni ya pesa ambao unasimamiwa na kampuni ya Ifaransa ya TOTAL.

Raia bado wayatoroka makaazi yao Palma

Maelfu ya wakaazi wa mji wa Pwani wa Palma nchini Msumbiji bado wanayakimbia makwao kwa kuhofia usalama wao baada ya magaidi kuvamia mlji huo wiki mbili zilizopita na kusababisha maafa.

Wakaazi hao wa Palma wamekimbilia mjini Pemba na wengi wao wanasema wanaogopa kurejea tena nyumbani.

Watu hawa waliotoroka makazi yaohuko Palma baada ya wanamgambo wa kiislamu kuvamia mji huo, wanasubiri ndugu zao kwenye bandari za Pemba, Tanzania,  mnamo Aprili 1, 2020.
Watu hawa waliotoroka makazi yaohuko Palma baada ya wanamgambo wa kiislamu kuvamia mji huo, wanasubiri ndugu zao kwenye bandari za Pemba, Tanzania, mnamo Aprili 1, 2020. REUTERS - STRINGER
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.