Pata taarifa kuu
CHAD

Chad: Kiongozi wa zamani wa waasi Baba Laddé ajiunga na rais Idriss Déby

Kiongozi wa zamani wa waasi nchini Chad, Abdelkader Baba Laddé, ametangaza kujiunga na rais wa nchi hiyo Idriss Déby. Kiongozi huyo wa waasi, ambaye alitoweka nchini Chad tangu kuachiliwa kwake huru, alionekana katika mkutano pamoja na rais wa Chad, huko Bongor, kusini mwa nchi.

Kiongozi wa zamani wa waaasi Abdelkader Baba Laddé.
Kiongozi wa zamani wa waaasi Abdelkader Baba Laddé. Page officielle Facebook
Matangazo ya kibiashara

Abdelkader Baba Laddé, ambaye anajulikana kwa jina la "mfalme wa msitu", ameelezea kilichopelekea anaungana na rais Idriss Deby.

"Nilifanya chaguo la amani. Hiyo ndiyo iliyonifanya nirudi. Sio kwa Chad tu bali kwa ukanda mzima. Unajua hii ni muhimu, unapozungumza kuhusu utulivu na amani, sio suala la mtu.

Kwa hivyo nimekuja kumuunga mkono Jemadari katika maono yake. Rais wa Jamhuri, mgombea kwenye kiti cha urais, aliomba nirudi. Alijaribu kunya kilio chini ya uwezo wake ili nirudi. Kwa hivyo, nimerudi nyumbani, kumsaidia tu kwa sababu anaendeleza kutunza amani na utulivu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.