Italia yataka UN kuchunguza mauaji ya balozi wake DRC
Serikali ya Italia, imesema imeomba Umoja wa Mataifa kuchunguza kwa kina kuuawa kwa Balozi wake Luca Attanasio, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wiki hii.
Imechapishwa:
Balozi Attanasio ambaye mwili wake umerejeshwa nyumbani, alishalbuliwa na watu wenye silaha wanaotuhumiwa kuwa wa FDLR karibu na mji wa Goma wakati alipokuwa katika msafara wa Shirika la mpango wa chakula duniani WFP.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Luigi Di Maio, katika hotuba yake kwa jopo la wabunge, alitoa maelezo ya awali ya namna shambulio hilo lilivyofanywa akisema washambuliaji sita wanadaiwa kuwa waliyaamuru magari katika msafara huo kusimama kwa kuweka vizuizi barabarani na kisha walifyatua risasi kadhaa hewani.
Katika shambulio hilo, dereva wa mwakilishi huyo ambaye pia ni raia wa wa Italia aliuawa. Waziri wa mambo ya kigeni wa Italia, Luigi Di Maio, aliliambia bunge la nchi yake kuwa wamewasilisha rasmi ombi kwa shirika la mpango wa chakula duniani pamoja na umoja wa mataifa kuanzisha upelelezi utakaobainisha klichotokea, hatua za kiusalama zilizochukuliwa na kubaini ni nani hasa aliyehusika na ukatili huo.