Pata taarifa kuu
TANZANIA- AFYA

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema serikali yake haijapiga marufuku uvaaji wa barakoa

Shirika la afya duniani, WHO, limetoa wito kwa Serikali ya Tanzania, kuchukua hatua za kukabiliana na maambukizi mapya ya Covid 19, wakati huu rais wa nchi hiyo John Magufuli, akikosolewa kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki kudhibiti maambukizi akidai ugonjwa huo ulimalizwa kwa njia ya maombi na kuendelea kutoa wito kwa wananchi wa taufa hilo kuendelea kuomba.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akiwahutubia wafuasi wa chama tawala CCM Makao makuu ya chama jijini Dar es Salaam.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akiwahutubia wafuasi wa chama tawala CCM Makao makuu ya chama jijini Dar es Salaam. REUTERS/Emmanuel Herman
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhenom Ghebreyesus, sasa anaitaka nchi hiyo  kutoa takwimu sahihi kuhusu mwenendo wa maambuki ya ugonjwa huo, akisema licha ya kuomba takwimu hizo mara kadhaa Serikali haijatoa ushirikiano.

Katika hatua nyingine, rais Magufuli, amekanusha madai ya kukataza watu kuvaa barakoa, badala yake amesema wahakikishe wanavaa barakoa sahihi.

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema: Ndugu zangu nchi nyingi zimeanza kuvaa barakoa.Nchi hizo ndizo zinaongoza kwa watu wengi kufa ; wengi maelfu. Sijasema msivae barakoa msinitafsiri vibaya, lakini kuna barakoa zingine sio nzuri nataka niwaambie huu ndio ukweli.Mtaletewa barakoa ambazo ndizo zenye matatizo. Mimi ni kiongozi wenu, ninajua mengi. Ukitaka kuvaa barakoa kavae zilizotengenezwa na wizara ya afya ; ukishindwa za namna hiyo shona yako mwenyewe, hii ni vita. Ninawaomba sana ndugu zangu wakristo ndugu zangu watanzania tujue Mungu yupo, tusiogope siku moja tutakufa, hata mimi nitakufa, na ndio maana mnaniona sijavaa barakoa sio kwamba siogopi kufa.

Rais Magufuli pia ameendelea kuwahimiza Watanzania kutumia njia mbadala katika kupambana na amaambukizi ya Virusi vya Corona ambayo aliitaja kuwa ni kujifukiza huku akiwataka wananchi wa Tanzania kutumia pia kufuata maelekezo ya wizara ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya kupumua yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.