Pata taarifa kuu
ALGERIA

Muuaji wa Hervé Gourdel ahukumiwa kifo

Abdelmalek Hamzaoui amehukumiwa kifo na mahakama ya Dar El Beïda kwa mauaji ya Hervé Gourdel, raia wa Ufaransa aliyeuawa mnamo mwaka 2014.

Waandamanaji nchini Algeria
Waandamanaji nchini Algeria Ramzi Boudina/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hamzaoui ni mshtakiwa pekee aliyekuwepo mahakamani wakati hukumu hiyo ikitolewa Alhamisi wiki hii.

Mawakili wake waliomba mteja wao aachiliwe huru wakibaini kwamba hana hatia yoyote.

Abdelmalek Hamzaoui alikuwa amekanusha mbele ya majaji kuhusika kwake katika mauaji ya Hervé Gourdel, aliyetekwa nyara na baadaye kukatwa kichwa mnamo mwaka 2014 katika mkoa wa Tizi Ouzou na kundi la kijihadi linalodai kuwa na mafungamano na kundi la Islamic State.

Alielezea kuwa alilazimishwa na mmoja kati ya jamaa zake kujiunga na kundi hilo la kijihadi. Maelezo yake hayakuzingatiwa na majaji ambao walifuunagna na hoja ya mwendesha mashtaka kuhusu hukumu hii ya kifo.

Mawakili wa vyama vya kiraia, walifanikiwa kuthibitisha kwamba Hamzaoui alionekana kwenye video inayomuonyesha mateka huyo kuwa yuko mikononi mwa kundi hilo la kijihadi. Na ushuhuda wa wakalimani wa Hervé Gourdel ulizidi kumuangamiza mshtumiwa.

Mashahidi kadhaa walithibitisha mbele ya mahakama kwamba Abdelmalek Hamzaoui alikuepo, silaha mkononi, wakati wanajihadi walipokuwa wakimpeleka Hervé Gourdel kwenda kuuawa.

Mashahidi hawa pia walikuwa wameshtakiwa kwa kuchelewa kutoa tahadhari baada ya kutekwa nyara kwa Mfaransa huyo, lakini wameachiliwa na mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.