Pata taarifa kuu
CHAD-UFARANSA

Mkutano wa G5 Sahel: Hatma ya Barkhane kujulikana

Mkutano wa kilele wa G5 Sahel unaanza Jumatatu hii, Februari 15 katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena kwa siku mbili mfululizo. Marais watano wa nchi za ukanda wa Sahel tayari wamewasili katika mji mkuu wa Chad.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ambaye atahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za G5 Sahel kupitia mtandao
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ambaye atahudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za G5 Sahel kupitia mtandao Lewis Joly / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuela Macron, ambaye amealikwa katika mkutano huo, atashiriki kwa njia ya video. Emmanuel Macron alisitisha ziara yake - kwa sababu za kiafya.

Hafla hiyo itafanyika katika awamu mbili: kwanza, mkutano halisi wa G5 Jumatatu hii mchana na kikao cha faragha ambapo rais wa Ufaransa atashiriki kwa njia ya video. Kesho Jumanne, nchi zinazosaidi ukanda wa Sahel kuwa tulivu Sahel, zitakutana kwa minajili ya kuweka mikakati pamoja.

Kuongeza kasi kwa yale yaliyofikiwa katika mkutano wa Pau, hilo ndilo lengo la mkutano huu wa N'Djamena, washirika wa karibu wa Emmanuel Macron wamebaini.

Miezi kumi na tatu iliyopita, katika mji huu wa Kusini Magharibi mwa Ufaransa, viongozi kutoka nchi za ukanda wa Sahel na Ufaransa waliamua kuhusu mpango wa kijeshi kuzingatia juhudi zao katika eneo linalojulikana kama "mipaka mitatu" kumlenga adui mmoja hasa, kundi la Islamic State katika ukanda wa Sahara.

Zaidi ya mwaka mmoja baadaye, Ikulu ya Élysée imekaribisha matokeo yaliyopatikana na kusema "mpango huu umezaa matunda dhidi ya adui" katika eneo hilo.

Lengo ni kuendelea na juhudi, yote hayo ni kutokana hasa na kuwasili kwa "bataliani moja ya wanajeshi wa Chad", ikulu ya rais imeongeza.

Wakati huo huo, Paris inataka kuongeza shinikizo kwa uongozi wa juu wa GSIM, kundi linaloongozwa na Iyad Ag Galy na kundi la Katiba Macina la Amadou Koufa.

Ufaransa inasema inataka "kuendeleza nguvu ya kijeshi kwa kutumia mpamno wa kisiasa na kiraia". Lengo ni kuzindua tena utekelezaji wa makubaliano ya Algiers na kuharakisha kurudi kwa utawala katika maeneo yaliyo hatarini zaidi.

Paris pia inatoa wito wa kutumia njia ya kidiplomasia kwa kuimarisha ushirikiano na nchi zinazopakana na Ghuba ya Guinea na kuhamasisha zaidi katika ngazi ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.