Pata taarifa kuu
CHAD

Chad: Waandamanaji 12 wahukumiwa kifungo kufuatia maandamano dhidi ya muhula wa 6 wa Déby

Watu 14 waliokamatwa Jumamosi ya wiki iliyopita wakati wakiandamana dhidi ya muhula wa sita wa rais Idriss Déby wamehukumiwa, baada ya kumi na wawili kati yao kukutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu, huku wengine wawili wakiachiliwa huru.

Rais wa Chad, Idriss Déby.
Rais wa Chad, Idriss Déby. ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Walikuwa 14 wakikabiliwa na mashitaka ya kujihusisha na vitendo viovu, vurugu zenye lengo la kuhatarisha usalama wa taifa, uharibifu na wizi wa mali za umma. Lakini mweka hazina wa chama cha Transformers, Fatimé Soumaïla, na mwanafunzi mmoja, waliachiliwa.

Wengine 12 walihukumiwa kwa kukaidi marufuku ya kuandamana Jumamosi ya wiki iliyopita, kufuatia uteuzi wa Idriss Déby kama mgombea kwa muhula wa sita katika uchaguzi wa urais ujao. Miongoni mwao, katibu mkuu wa shirika la Haki za Binadamu, Mahamat Nour Ibedou. Shirika lake limelaani hukumu hiyo likisema ni hukumu ya kisiasa isio kuwa na msingi wa kisheria.

Hayo yanajiri wakati kundi lililoitisha maandamano ya Jumamosi iliyopita, limeitisha maandamano mapya leo Jumamosi na Jumatatu wiki ijayo. Haijafahamika iwapo maandamano hayo yataitikiwa na watu wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.