Pata taarifa kuu
MALI-ALGERIA

Kamati ya Ufuatiliaji ya Mkataba wa Algiers kufanyika Kidal, Mali tangu 2015

Mkutano wa Kamati ya Ufuatiliaji wa Amani ya Algiers (CSA) unatarajia kufanyika huko Kidal, nchini Mali, leo Alhamisi Februari 11. Huu ni mkutano wa kwanza tangu kusainiwa kwa mkataba mnamo mwaka 2015 kati ya wadau wote nchini Mali.

Wanajeshi wa Ufaransa wakifanya doria kwenye mji wa Gao
Wanajeshi wa Ufaransa wakifanya doria kwenye mji wa Gao REUTERS/Emmanuel Braun
Matangazo ya kibiashara

Mbele ya wanadiplomasia kadhaa wa Kiafrika na Ulaya, ambao nchi zao ni wanachama wa kamati hiyo, pande zilizotia saini kwenye mkataba huo wanataka kushughulikia kujadili maswala muhimu ili kuwezesha utekelezwaji wake.

 

Mwezi Septemba 2019, mkutano wa CSA uliopangwa huko Kidal, jiji hili la Mali ambalo bado liko mikononi mwa waasi wa zamani, ulifutwa katika dakika za mwisho, hali ambayo ilikasirisha sana viongozi wenye ushawishi mkubwa wa jiji hilo.

 

Wakati huu, wajumbe wakuu wa CSA - makundi ya waasi na upande wa serikali - wamesema wako tayari kushiriki mkutano huo.

 

Mamlaka ya kiraia na ya kijeshi ya mpito imethibitisha taarifa hiyo, sasa wanataka kuwa na uhusiano usio na kizuizi na makundi ya waasi yaliyohusika katika mchakato wa amani.

 

Wengi wanaona kwamba makubaliano kuhusu mkutano huu unaotarajia kufanyika leo katika mji wa Kidal ni ishara nzuri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.