Pata taarifa kuu
MOROCCO

Morocco: 28 wafariki katika mafuriko ya kiwanda haramu Tangier

Takriban watu 28 wamekufa baada ya mafuriko katika kiwanda cha nguo kisichotambuliwa na mamlaka nchini Morocco, kwa mujibu wa vyanzo vya serikali, vikinukuliwa na shirika la habari la REUTERS.

Wahamiaji wa Afrika wakiwa kaika fukwe ya Morocco
Wahamiaji wa Afrika wakiwa kaika fukwe ya Morocco AFP PHOTO / FADEL SENNA / AFP PHOTO / FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Kiwanda hiki kinapatikana chini ya nyumba moja huko Tangier, mamlaka nchini Morocco imebaini, na kuongeza kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kujua wahusika wa kiwanda hiki.

Maafisa wa usalama wamesema kuwa watu 18 wameokolewa katika shughuli ya uonkoaji inayoendelea katika eneo la tukio.

Kazi isiyo rasmi nchini Morocco inachukua karibu theluthi moja ya shughuli za kiuchumi zisizo za kilimo na wafanyakazi mara nyingi wanakabiliwa na mazingira magumu ya kufanya kazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.