Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Waasi 44 wauawa na vikosi vya Afrika ya Kati na washirika wao

Vikosi vya jeshi vya Afrika ya Kati vilichukua udhibiti wa mji wa Boda, ulioko kilomita 180 kusini magharibi mwa Bangui, katika mkoa wa Lobaye, ambapo waasi wa CPC walikuwa wamepiga kambi kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Wanajeshi wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
Wanajeshi wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati REUTERS/Antoine Rolland
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati, FACA, na vikosi vya washirika pia walifanya shambulio siku ya Jumapili karibu na kijiji cha Lambi.

Kulingana na mamlaka, watu 44 waliuawa upande wa waasi wa CPC, na kubaini kwamba wamewasafirisha wafungwa watatu kwenda katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.

Jamjuri ya afrika ya Kati imeendelea kukumbwa na mapigano kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi, tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi nchini humo.

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, François Bozize, amendelea kunyooshewa kidole cha lawama kwamba anahusika katika kuhatarisha usalama wa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.