Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Kamanda wa zamani wa Seleka akabidhiwa ICC

Kamanda wa zamani wa vikosi vya zamani vya Seleka yuko mikononi mwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) tangu Jumapili jioni. Hatua iliyochukuliwa na mamlaka nchini Afrika ya Kati .

Waasi wa Seleka mwaka 2014
Waasi wa Seleka mwaka 2014 REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Mahamat Said Abdel Kani, anashukiwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Ni kiongozi wa kwanza wa kundi la zamani la waasi wa Seleka kukabidhiwa kwa ICC.

Waranti wa kukamatwa wa ICC dhidi ya Mahamat Said Abdel Kani ulitolewa mwezi Januari 2019. Kwa hiyo ilikuwa ni miaka miwili tangu mahakama hiyo ya kimataifa ilipotaka akamatwe.

Baada ya kukamatwa Jumatano wiki iliyopita, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu iliomba mamlaka ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kumkabidhi mshutumiwa huyo.

Said Abdel Kani alikamatwa Jumatano Januiari 20, huko Bria, mahali alipozaliwa, mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mahamat Said Abdel Abdel Kani, mwenye umri wa miaka 50, inasemekana mwaka 2013, alikuwa karibu Michel Djotodia, wakati huo mkuu wa Seleka wakati wa machafuko ya umwagaji damu katika vita dhidi ya wanamgambo wa anti-balaka, baada ya kupinduliwa kwa rais wa zamani François Bozizé.

Baadaye, alikuwa afisa mwenye ushawishi mkubwa wa kundi la FPRC la Noureddine Adam, moja wapo ya makundi yaliyozaliwa tangu kuvunjika kwa kundi la waasi wa zamani wa seleka mwishoni mwa mwaka 2014.

Hivi karibuni, kulingana na mmoja wa wasemaji wa FPRC, "hakushikilia tena wadhifa wa kijeshi" na "alikuwa amerudi kwenye siasa". Alikuwa mgombea kwenye nafasi ya ubunge katika uchaguzi wa mwezi Desemba.

Maelezo ya mashtaka yake bado hayajajulikana. Lakini ICC inamshuku kuhusika na makosa kadhaa ikiwa ni pamoja na uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.