Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Kikosi cha MINUSCA chawatimua waasi katika mji wa Bangassou

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wameudhibiti tena mji wa Bangassou wenye utajiri wa madini ya almasi, ulio umbali wa Kilomita 750 kutoka jiji kuu la Bangui, uliokuwa umetekwa na waasi.

Mji wa  Bangassou nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
Mji wa Bangassou nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Alexis HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kikosi hicho cha MINUSCA kinasema mji huo sasa iko mikononi mwao na kipo macho kuhakikisha kuwa hakuna uvamizi mwingine kutoka kwa waasi unaotokea.

Wakati hayo yakijiri, Askofu wa Kanisa Katoliki katika jimbo la Bosangoa Nestor Desire Nongo, ameendelea kutoa wito wa amani katika nchi hiyo katika kipindi hiki.

Waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa mara ya kwanza mapema mwezi Janauri waliuteka mji wa Bangassou, masharaki mwa mji mkuu Bangui, siku moja kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais na bunge ulioitishwa Desemba 27.

Hayo yanajiri wakati shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa nchini DRC, hivi karibuni, lilisema lilisitisha zoezi la kuwarejesha wakimbizi wa Jamhuri ya Afrika ya kati waliokuwa wakiishi nchini Kongo.

Wakimbizi hao ambao walikimbia vita miaka mitatu iliopita walikuwa wakiishi kwenye miji ya Zongo na Libenge jimboni Sud-Ubangi kaskazini magharibi mwa Kongo.

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa lilisema wakimbizi 5,200 waliokuwa wakiishi DRC walirejeshwa nchini mwao tangu Januari mwaka 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.