Pata taarifa kuu
DRC

UNICEF yataka kufunguliwa tena kwa shule nchini DRC

Tangu Desemba 18, wanafunzi nchini Jamhuri ya Kidemukrasia ya Congo wako nyumbani. Uamuzi huu ulichukuliwa ili kuzuia kuenea kwa mlipuko wa pili wa janga la Corona.

Nembo ya UNICEF
Nembo ya UNICEF REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Licha ya uamuzi huo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema, serikali lazima sasa itoe kipaumbele kwa kufungua tena shule, ikichukua hatua zote kulinda wanafunzi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linabaini kwamba uamuzi wa kufunga shule nchi nzima unapaswa kuepukwa iwezekanavyo. UNICEF ​​inasema kuwa uamuzi huu unapaswa kuwa hatua ya mwisho tu, baada ya hatua zingine zote kushindwa.

Shirika lhilo linaangazia hasa kesi ya watoto waliotengwa kifamilia, ambao wanasemekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kuacha masomo kabisa. Yote hayo ni athari ya kufungwa kwa shule nchini humo, UNICEF imeongeza .

UNICEF ​​inataja tafiti zilizofanywa hivi karibuni nchini DRC ambazo zinaripoti kupunguwa kwa idadi ya wanafunzi shuleni, hasa wasichana wakati mwaka wa shule wa 2020-2021 ulipoanza.

Serikali, kwa upande wake, inasisitiza kuwa hali ya kiafya hairuhusu kufunguliwa kwa shule. "Tunafanya juhudi kudhibiti idadi ya vifo, lakini idadi ya watu wanaokufa [kutokana na COVID-19] inaanza kuongezeka", amesema Waziri wa Afya, Daktari Eteni Longondo.

Shule zitafunguliwa tena, lakini hakuna tarehe iliyopangwa kufikia sasa, amesema. "Wanafunzi wasifikirie kuwa hawatasoma, watasoma, ni suala tu la wakati," ameongeza waziri huyo.

UNICEF inasema ikiwa watoto watakaa muda mrefu bila kwenda shule, athari itakuwa upande wa vizazi kadhaa vijavyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.