Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Wagombea kumi wataka uchaguzi wa urais ufutwe

Wagombea urais kumi kati ya kumi na sita wamesema katika taarifa kwamba hawatambui matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais wa Desemba 27, 2020 na wanataka uchaguzi huo "kufutwa."

Kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia
Kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Michel Djotodia Florent Vergnes / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu wiki hii, Tume ya Uchaguzi (ANE) ilimtangaza rais anayemaliza muda wake Faustin-Archange Touadéra kushinda uchaguzi huo katika duru ya kwanza kwa zaidi ya 53% ya kura zilizopigwa.

Matokeo ambayo yalihusu nusu tu ya wapiga kura. Nusu nyingine haikuweza kupiga kura kutokana na mashambulio ya waasi yanayoendelea nchini.

Wagombea hao kumi wamebaini kwamba uchaguzi wa urais wa Desemba 27 ni "pingamizi kubwa kwa demokrasia", na wamekiri kuwa hawatokubali 'ushindi na uhalali' wa rais aliyetangazwa mshindi na kuomba uchaguzi huo ufutwe.

Kwa kuunga mkono ombi lao, wamelaani "kasoro nyingi" ambazo, kulingana na wagombea hao, ziligubika uchaguzi.

Kiwango rasmi cha ushiriki kilichotangazwa Jumatatu jioni kilikuwa 76.31% kulingana na hesabu za Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (ANE), licha ya kutozingatia nusu ya wapiga kura, sawa na wapigakura 910,000 kati ya jumla ya wapiga kura milioni 1.8 waliojiandikisha ambao walizuiwa kupiga kura.

Katika maeneo mbalimbali watu hawakupiga kura kwa sababu mbalimbali. katika baadhi ya maeneo zoezi la kupiga kura halikufanyika, na katika maeneo mengine kadi za kupigia kura zilichomwa," amebaini Théophile Momokoama, mmoja wa maafisa wa Tume ya Uchaguzi ANE alisema.

Kwa mujibu wa matokeo hayo kiongozi wa upiunzani Anicet-Georges Dologuélé alipata asilimia 21.01, akifuatiwa na mwanasiasa mwengine Martin Ziguele katika nafasi ya tatu ambaye amepata asilimia 7.46%.

Upinzani una siku 3 tangu kutangazwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi kukata rufaa kwa Mahakama ya Katiba, ambayo kwa upande wake ina hadi Januari 19 kuzichunguza na kutangaza matokeo ya mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.