Pata taarifa kuu
MEXICO-DRC

Mexico: Wahamiaji kutoka DRC na Haiti waendelea kukumbwa na madhila mbalimbali

Wahamiaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Haiti waliokwama kwenye mpaka wa Mexico bado wana ndoto ya kuingia nchini Marekani licha ya changamoto nyingi wanazopitia kwenye mpaka huo.

Wahamiaji toka bara la Amerika Kusini wakijaribu kuingia Marekani.
Wahamiaji toka bara la Amerika Kusini wakijaribu kuingia Marekani. Pedro PARDO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu kufungwa kwa mpaka kwa sababu ya ugonjwa hatari wa COVID-19 na chini ya sheria iliyowekwa na utawala wa Trump, maelfu ya Waafrika na raia kutoka eneo la Caribbean wamekwama nchini Mexico.

 

Wahamiaji hao ambao wamezuiliwa kuingia nchini Marekani wakati ombi lao la ukimbizi lilishughulikiwa, kutokana na hali ngumu ya maisha na ukosefu wa chakula, wameanza kuranda randa mitaani.

 

Sera ya mpaka wa Marekani ni moja wapo ya faili ambazo zitalazimika kushughulikiwa na utawala mpya wa Joe Biden, ambaye anatarajia kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi Januari 20.

 

 Wakati Donald Trump alipoingia madarakani mnamo mwaka 2016, mawakili 20,000, pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu, waliunda chama cha Mawakili, Lawyers for Good Government Foundation. Moja ya miradi yao ni kuwasaidia wahamiaji huko Matamoros.

 

Kambi ya wahamiaji huko Matamoros ilikuwa na watu 3,000 kabla ya janga la COVID-19, na kwa wahamiaji 1,000 tu ndio wamesalia katioka kambi hiyo. Wahamiaji wengi kutoka Uhispania walifaulu kuondoka na kwenda mahali pengine. wahamiaji walioko katika kambi hiyo ni kutoka DRC, Cameroon, Angola na Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.