Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Jean-Pierre Lacroix akutana kwa mazungumzo na Félix Tshisekedi

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani Jean-Pierre Lacroix, ambaye yuko ziarani nchini DRC, amekutaka kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo, Félix-Antoine Tshisekedi.

Rais wa DRC, Felix Tshisekedi
Rais wa DRC, Felix Tshisekedi ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wamejadili kuhusu jinsi ya kuwasaidia raia wa DR Congo kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Suala la ukosefu wa usalama mashariki mwa nchi, hali ngumu ya kijamii na kiuchumi na matatizo ya kibinadamu vimetawala mazungumzo kati ya wawili hao, ambao wamejadili kuhusu njia ambayo Umoja wa Mataifa unapanga kuendeleza ushirikiano wake na DRC, na kusaidia raia wa nchi hiyo.

Wamezungumzia pia juu ya athari za janga la COVID-19, ugonjwa ambao, kulingana na rais Tshisekedi, uko katika awamu yake ya pili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Félix Tshisekedi amembainishia mgeni wake wa heshima maono yake kuhusu hali ya kisiasa ya sasa nchini DRC, na jinsi anavyopanga kuishughulikia.

Jean-Pierre Lacroix anasema amekaribisha mazungimzo hayo na yale kuhusu hatima ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Drc, MONUSCO, ambayo muhula wake unamalizika hivi karibuni nchini humo.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani amebaini kwamba askari wa umoja aw Mataifa nchini DRC wataondoka nchini humo hatua kwa hatu kulingana na hali itakavyokuwa kuwa ikijiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.