Pata taarifa kuu
LIBYA-UTURUKI-USALAMA-SIASA

Uturuki yataka kuongeza muda kwa wanajeshi wake kusalia nchini Libya

Ofisi ya rais nchini Uturuki iliwasilisha Bungeni Jumamosi hii, Desemba 12 azimio la kuongeza muda kwa wanajeshi wake waliopelekwa Libya kusalia nchini humo.

Kiongozi wa vikosi vya upinzani nchini Libya  Khalifa Haftar
Kiongozi wa vikosi vya upinzani nchini Libya Khalifa Haftar REUTERS/Esam Omran Al-Fetori/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na azimio hilo, muda wa wanajeshi wa Uturuki kusalia nchini Libya umeongezwa kwa miezi 18 zaidi, ili kusaidia serikali ya umoja wa kitaifa.

Azimio hilo litajadiliwa katika siku zijazo. Kupitishwa kwake hakuna shaka, kutokana na idadi kubwa ya wabunge wa chama kilicho madarakani na mshirika wake.

Mapema mwaka huu, Uturuki ilituma wanajeshi nchini Libya kusaidia serikali ya umoja wa kitaifa dhidi ya majeshi ya Marshal Khalifa Haftar.

Kupelekwa kwa wanajeshi wa Uturuki nje ya nchi kunahitaji idhini kutoka Bunge la nchi hiyo na muda wa wanajeshi hao kusalia nchini Libya unamalizika Januari 2, 2021.

Rais Erdogan anaomba wabunge kurejemea upya muda huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.