Pata taarifa kuu
SAHARA MAGHARIBI-MOROCCO-MAREKANI

Chama cha Polisario chalaani msimamo wa Marekani juu ya Sahara Magharibi

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza Alhamisi, Desemba 10 kwamba Moroco na Israel zimeamua kurejesha tena uhusiano wao, na kutangaza pia kwamba Marekani inatambua uhuru wa Morocco juu ya Sahara Magharibi.

Wanajeshi wa  Sahara Magharibi, eneo ambalo lina mzozo na Morocco
Wanajeshi wa Sahara Magharibi, eneo ambalo lina mzozo na Morocco FAROUK BATICHE/AFP via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Msimamo huu wa Marekani ni uungwaji mkubwa wa kidiplomasia kwa Rabat lakini ni msimamo ambao unaonekana kwenda kinyume na msimamo wa UMoja wa Mataifa.

Wakati mapigano yameanza kurindima tena tangu mwezi uliopita katika eneo la Sahara Magharibi, Morocco innaonekana kupata ushindi wa kidiplomasia wa kiwango cha juu wa utambuzi wa Marekani kuhusu uhuru wake kwa eneo hilo.

Hata hivyo, Chama cha Polisario Front kimefutilia mbali uamuzi huo wa Marekani, kulingana na Oubi Bouchraya Bachir, mwakilishi wa chama hicho barani Ulaya na Umoja wa Ulaya.

"Ni uamuzi unaokwenda kinyume na usalama na utulivu wa kikanda [...] ambao kwa hakika utakuwa na athari mbaya kwa juhudi za Umoja wa Mataifa za kutafuta suluhisho la mzozo huo, " amesema Oubi Bouchraya Bachir.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.