Pata taarifa kuu
IVORY COAST

Laurent Gbagbo apewa hati zake za kusafiria za Côte d’Ivoire

Rais wa zamani wa Côte d’Ivoire anatarajia kurudi nchini humo hivi karibuni, baada ya kusubiri kwa miezi kadhaa, Laurent Gbagbo hatimaye amepata hati zake mbili za kusafiria.

Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, hapa ilikuwa Uholanzi, tarehe 6, Februari 2020.
Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, hapa ilikuwa Uholanzi, tarehe 6, Februari 2020. Jerry Lampen/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tangu kukamatwa kwake Aprili 2011, Laurent Gbagbo hakuwa tena na hati ya kusafiria.

 

Mapema leo Ijumaa asubuhi, saa 11 alfajiri, katika hoteli kubwa kwenye mtaa wa Louise huko Brussels, rais wa zamani wa Côte d’Ivoire alipewa pasipoti ya kawaida na pasipoti ya kidiplomasia.

 

Pasipoti hizo lililetwa na wanadilpmasia wawaili kutoka Côte d’Ivoire: mjumbe maalum kutoka Abidjan, Mkurugenzi katika Wizara ya Mambo ya nje, na Balozi wa Cote d'Ivoire nchini Ubelgiji.

 

Mwezi Julai mwa huu rais wa zamani wa Côte d’Ivoire alianzisha taratibu wa kupata hati hizo mbili alizokuwa nazo kabla. Familia yake na watu wake wa karibu walikasirishwa mara kadhaa na ucheleweshaji wa kutoa pasipoti zake.

 

Hata hivyo mambo yalionekana kushika kasi wiki iliyopita baada ya timu kutoka Wizara ya Mambo ya nje kusafiri kwenda Brussels ili kuwasajili wanadiplomasia kadhaa na rais wa zamani Laurent Gbagbo. Zoezi hilo lilifanyika katika hoteli moja huko Brussels: alama za vidole, picha na kukabidhi nyaraka muhimu kwa mchakato huu.

 

Duru za kuaminika zinabaini kwamba Laurent Gbagbo anatarajia kurudi nchini Côte d’Ivoire mwishoni mwa mwezi huu wa Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.