Pata taarifa kuu
UN-COVID19

Coronavirus: Umoja wa Mataifa watiawa hofu na kuongezeka kwa visa vya maambukizi duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa dunia huenda ikaendelea kupambana na janga la Corona kwa muda mrefu sana licha ya kuwepo kwa habari njema ya matumaini ya kupatikana kwa chanjo ambazo zipo katika mchakato wa kuthibitishwa iwapo zipo salama.

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. RFI
Matangazo ya kibiashara

Guteress amewaambia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliokutana kwa mara ya kwanza kupitia mtandao kujadili janga la Corona kuwa, inasikitisha dunia haijaungana kupambana dhidi ya janga hili.

Janga la Corona limesababisha vifo vya watu Milioni Moja na Laki Tano kote duniani na wengine Milioni 65 wameambukizwa.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

 

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.