Pata taarifa kuu
CAR-UN-AU-USALAMA

UN, AU na ECCAS wakamilisha ziara yao ya pamoja Jamuhuri ya Afrika ya Kati

Ujumbe wa pamoja wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani Jean-Pierre Lacroix, Kamishna wa masuala ya Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Balozi Smail Chergui na rais wa Tume ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Kati, Balozi Gilberto da Piedade Veríssimo umekamilisha ziara yake Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani, Jean-Pierre Lacroix, amekamilisha ziara ya siku tatu nchini jamhuri ya Afrika ya Kati Ijumaa hii (picha ya kumbukumbu)
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani, Jean-Pierre Lacroix, amekamilisha ziara ya siku tatu nchini jamhuri ya Afrika ya Kati Ijumaa hii (picha ya kumbukumbu) Samuel HABTAB / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo ulikutana na rais wa Jamhuri, viongozi wa kidini, wawakilishi wa mashirika ya kiraia na makundi vyenye silaha ... Utekelezaji wa makubaliano ya amani ilikuwa moja ya mada kuu ya ziara hii.

Makundi aliyotia saini kwenye mkataba wa amani yameelezea kutoridhika kwao mara kadhaa. Siku mbili zilizopita, makundi hayo yalitoa hati nyingine inayoelezea kile wanachoamini kiinazuia utekelezaji wa mkataba huo amani: kutofanya kazi kwa vyombo vya utekelezaji, uamuzi wa upande mmoja, viongozi na wawakilishi wa makundi yenye silaha wanaolengwa au kudharauliwa ...

Jean-Pierre Lacroix anakiri kuwa katika baadhi ya mambo yaliyoafikiwa kumekuwa na ucheleweshaji. Hasa, kuundwa kwa vitengo maalum vya usalama wa pamoja, vitengo hivi ambavyo vinapaswa kuundwa kwa sehemu moja na wapiganaji wa zamani na vikosi vya ulinzi na usalama, kulingana na mkataba wa amani. Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani Jean-Pierre Lacroix amebaini: "Ahadi bado zinahitaji kutimizwa kikamilifu".

Hata hivyo vurugu za makundi yenye silaha zinaendelea, na vile vile ukiukaji wa mkataba wa amani, ingawa kwa sasa ukiukwaji huo unaonekana kupungua. Mwezi Juni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema ana wasiwasi sana na mapigano makali yanayoendelea ambayo yanahusisha makundi yenye silaha na kusababisha machafuko dhidi ya raia na wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.