Pata taarifa kuu
ALGERIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Rais wa Algeria ahamishiwa hospitali nchini Ujerumani

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune amehamishiwa katika hospitali moja nchini Ujerumani kwa uchunguzi wa kimatibabu, vyombo vya habari vya serikali viliripoti Jumatano wiki hii, kulingana na shirika la habari la REUTERS.

Rais mpya wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune, wakati wa kuapishwa kwake huko Algiers, Desemba 19, 2019.
Rais mpya wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune, wakati wa kuapishwa kwake huko Algiers, Desemba 19, 2019. RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Abdelmadjid Tebboune alijiweka karantini siku ya Jumamosi baada ya kuwasiliana na watu waliokuwa na dalili za virusi vya COVID-19, bila kubaini, hata hivyo, ikiwa rais mwenyewe ameambukizwa.

Wakati huo alilazwa katika kitengo maalum cha hospitali ya jeshi ya Algeria.

Abdelmadjid Tebboune, mwenye umri wa miaka 75, alimrithi rais Abdelaziz Bouteflika karibu mwaka mmoja uliopita, akishinikizwa kuachia madaraka na maandamano makubwa yaliyoikumba nchi hiyo.

"Ninawahakikishia, ndugu zangu na dada zangu, kwamba mimi ni mzima na kwamba ninaendelea na majukumu yangu", rais Abdelmadjid Tebboune ametangaza kulingana na vyombo vya habari vya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.