Pata taarifa kuu
MAREKANI-SUDAN-USHIRIKIANO

Sudan kuondolewa kwenye orodha ya mataifa yanayounga mkono ugaidi

Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kuiondoa Sudan kwenye orodha yake ya mataifa yanayofadhili ugaidi duniani baada ya nchi hiyo kukubali kufidia familia za wahanga wa Marekani wa mashambulizi yaliyofanywa mwaka 1998 barani Afrika.

Trump ametoa tamko hilo ikiwa zimebakia takriban wiki mbili hadi siku ya uchaguzi mkuu wa Marekani.
Trump ametoa tamko hilo ikiwa zimebakia takriban wiki mbili hadi siku ya uchaguzi mkuu wa Marekani. Tia Dufour/The White House via AP
Matangazo ya kibiashara

"Habari njema! Serikali mpya ya Sudan, ambayo inafanya maendeleo ya kweli, imekubali kulipa dola milioni 335 kama fidia kwa wahanga wa Marekani wa ugaidi na familia zao.

Mara baada ya kulipwa, nitaiondoa Sudan kwenye orodha ya mataifa yanayofadhili ugaidi, ” rais wa Marekani ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Tangazo hili linakuja baada ya miezi kadhaa ya majadiliano kati ya serikali ya mpito ya Sudan na uongozi wa Marekani, rais Trump akisema ataiondoa Sudan kwenye orodha hiyo mara tu baada ya Sudan kulipa fidia hiyo.

 Muda mfupi baada ya matamshi ya Trump, waziri mkuu wa Sudan Abdallah Hamdock alijibu kwa kusema kuwa tayari fedha hizo zimehamishwa, na kile wanachosubiri ni uthibitisho kutoka kwa mamlaka ya Marekani.

Trump ametoa tamko hilo ikiwa zimebakia takriban wiki mbili hadi siku ya uchaguzi mkuu wa Marekani.

Hatua hiyo itafungua milango kwa nchi hiyo ya Afrika kupata mikopo ya kimataifa na misaada inayohitajika kufufua uchumi wake uliporomoka pamoja na kuisaidia nchi hiyo kuwa ya kidemokrasia.

Marekani ilichukua uamuzi wa kuiweka Sudan katika orodha hiyo mnamo mwaka 1993, ikiamini rais wa wakati huo Omar al-Bashir alikuwa akifadhili makundi ya kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.