Pata taarifa kuu
MAURITANIA-MAJANGA ASILI

Mafuriko makubwa yaathiri mashariki mwa Mauritania

Katika miji ya mashariki mwa Mauritania karibu na mpaka na Mali, mvua kubwa imesababisha hasara kubwa, huku raia wakisalia bila makazi.

Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh el-Ghazouani kwenye mkutano wa Pau kuhusu hali ya Sahel, Januari 13, 2020.
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh el-Ghazouani kwenye mkutano wa Pau kuhusu hali ya Sahel, Januari 13, 2020. REGIS DUVIGNAU / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akiandamana na wajumbe kadhaa wa serikali, Rais Ghazouani alifanya ziara katika miji hii miwili siku ya Alhamisi na Ijumaa ili kujionea mwenye hasara iliyosababishwa na mfua hizo.

Ameahidi misaada ya serikali kupunguza mateso yanayowakabilia watu walioathiriwa tukio hilo na kuanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ili kuingia katika miji ambayo si rahisi kufika wakati wa mvua. Lakini mji wa Bassiknou, ulioathiriwa vibaya na mafuriko hayo, ndio umepewa kipaumbele.

Kulingana na Ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA, karibu watu 760,000 wameathiriwa na mafuriko ambayo yameshambulia nchi kadhaa za Afrika Magharibi na sehemu za Afrika ya Kati kwa wiki kadhaa.

Mvua kubwa zilizonyesha mwaka jana zilisababisha mafuriko makubwa, na kuathiri zaidi ya watu milioni moja katika nchi kumi na moja.

Ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA inasema ina wasiwasi kuwa takwimu hii inaweza kuzidi mwaka huu kwa sababu msimu wa mvua haujaisha.

Mji wa Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso unakumbwa na mafuriko kwa muda wa wiki moja. Serikali ya Burkina Faso, imebaini kwamba watu kumi na tatu wamepoteza maisha na hivyo kutangaza hali ya janga la asili jana Jumatano.

Nchini Ghana, pia, mvua kubwa na kuongezeka kwa kiwango cha maji vimeua watu kadhaa kaskazini mwa nchi.

Hali kama hiyo nchini Nigeria ambapo majimbo ya kaskazini ndiyo yameathirika zaidi. Ofisi ya uratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA imeripoti watu 30 waliopoteza maisha, jimbo la Borno pekee limeripoti watu 26,000 ambao hawana makazi baada ya nyumba zao kusombwa na maji.

Hali ya kutisha nchini Sudan

Lakini Niger ndio imeathirika zaidi kutokana na mafuriko haya katika eneo hilo dogo lenye watu 330,000 walioathirika, 65 wamepoteza maisha na nyumba 34,000 zimeharibiwa, kulingana na takwimu zilizotolewa Jumatano na Waziri wa Haki za Kibinadamu wa Niger na uratibu wa majanga. Katika eneo la Mashariki, Chad na Cameroon pia zinakabiliwa na kuongezeka kwa viwango vya maji baharini, lakini hali ni ya kutisha zaidi nchini Sudan. Waziri wa Mambo ya nje wa Sudan anakadiria kuwa watu 500,000 wanaweza kuathiriwa moja kwa moja na mafuriko hayo ambayo yamesababisha vifo vya watu 101.Hali ya hatari ilitangazwa Ijumaa kwa miezi mitatu kote nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.