Pata taarifa kuu
MALI-MINUSMA-SIASA-USALAMA

MINUSMA yachunguza vifo wakati wa maandamano na wakati wa mapinduzi Mali

Maswali yanaendelea kuongezeka kuhusu mabadiliko ya kisiasa, kuhusu matukio ya wiki za hivi karibuni, na kuhusu mazingira ambamo wananchi wa Mali waliuawa. Iwe kabla ya mapinduzi, wakati wa ukandamizaji wa maandamano ya serikali ya wakati huo, lakini pia wakati wa mapinduzi ya kijeshi, Agosti 18.

Wanajeshi wa Mali katika kambi ya Kati, Agosti 19, 2020.
Wanajeshi wa Mali katika kambi ya Kati, Agosti 19, 2020. ANNIE RISEMBERG / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kitengo cha haki za binadamu cha Tume ya Umoja wa Mataifa nchini mali, MINUSMA, kimeanzisha uchunguzi ili kujaribu kuondoa sintofahamu inayoendelea kuhusu matukio hayo. Uchunguzi huu bado haujakamilika lakini RFI imepata sehemu ya kwanza ya hitimisho.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu nchini Mali, watu watatu waliuawa huko Kayes, mmoja huko Sikasso, kumi na wanne huko Bamako, na zaidi ya 150 walijeruhiwa katika ukandamizaji wa siku kadhaa za maandamano yaliyotangulia kuanguka kwa utawala wa rais wa zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, kulingana na uchunguzi uliofanywa na wachunguzi kutoka MiNUSMA, kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini.

Watu hao waliuawa na vikosi vya usalama vya Mali: polisi, na kikosi cha kupambana na ugaidi (FORSAT), ambapo wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanahoji kwa nini vikosi hivyo vilitumia nguvu za kupita kiasi na kusababisha mauaji hayo.

MINUSMA pia inachunguza kuhusu waathiriwa wa siku ya mapinduzi: wakati wanajeshi wa Baraza la Kitaifa la Wokovu (CNSP) walijipongeza kwa kufanikiwa kwa mapinduzi 'bila umwagaji damu', wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanabaini kwamba karibu watu kumi na tano walijeruhiwa na wanne waliuawa. Watatu waliuawa mbele ya jengo la Wizara ya Bajeti, mmoja nyumbani kwa Karim Keïta, mtoto wa rais aliyetimuliwa madarakani IBK na mbunge wa zamani wa Kamati ya Ulinzi katika Bunge la Mali.

Kulingana na uchunguzi wa awali kikosi cha ulinzi wa kitaifa, kilichotumwa na kundi la wanajeshi lililofanya mapinduzi, ndio wanadaiwa kuwapiga risasi watu hao. "Labda ilikuwa kujaribu kuzuia uporaji," amesema mmoja wa wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, ambaye bado anasubiri maelezo kutoka kundi la wanajeshi waliofanya paminduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.