Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-GBAGBO-SIASA

Mahakama Cote d'Ivoire: Laurent Gbagbo hana nafasi ya kuwania katika uchaguzi wa urais

Rais wa zamani Laurent Gbagbo amefutwamoja kwa moja kwenye orodha ya wagombea urais nchini Cote d'Ivoire. Mahakama ya mwanzo ya Plateau jijini Abidjan imethibitisha uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi uliyotolewa wiki iliyopita.

Laurent Gbagbo, katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai huko Hague, Januari 15, 2019.
Laurent Gbagbo, katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai huko Hague, Januari 15, 2019. Peter Dejong/Pool via REUTERS/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa zimesalia siku tano kabla ya tarehe ya mwisho ya kuwasilisha fomu za wagombea katika uchaguzi wa urais, mahakama nchini Cote d'Ivoire imethibitisha kuwa Laurent Gbagbo hana nafasi ya kuwania kwenye kiti cha uras katika uchaguzi huo.

Hakuna rufaa inayowezekana mbele ya mahakama ya juu ya Cote d'Ivoire.

Uchaguzi wa urais chini Cote d'Ivoire umepangwa kufanyika Oktoba 31. Mahakama ya mwanzo ya Plateau huko Abidjan, baada ya kupata barua kutoka mawakili wa rais wa zamani, imethibitisha Jumanne Agosti 25 uamuzi wa Tume ya Uchaguzi kwamba Laurent Gbagbo hana nafasi ya kuwania katika uchaguzi wa urais ujao.

Sababu ya Laurent Gbagbo kuondolewa kwenye orodha ya wagombea urais ni kutokana na hukumu dhidi yake iliyotolewa na mahakama ya Cote d'Ivoire ya kifungo hadi miaka 20 jela katika kesi inayojulikana kama "wizi wa fedha katika benki kuu ya jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, BCEAO. Wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa 2010-2011, serikali yake, ambayo ilikuwa chini ya vikwazo vya fedha, ilitumia fedha kutoka Benki Kuu ya jumuiya hiyo ya ECOWAS, BCEAO.

Baada ya kukataliwa na Tume Huru ya Uchaguzi (CEI) kisha na mahakama ya Cote d'Ivoire, wakili wa rais huyo wa zamani anafikiria uwezekano wa kuwasilisha malalamiko yake mbele ya mahakama kikanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.