Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-GBAGBO-USALAMA-SIASA

Simone Gbagbo avunja ukimya na kumuomba rais amsamehe mumewe arejee nchini

Simone Gbagbo mke wa rais wa zamani wa Côte d’Ivoire, Laurent Gbagbo amemtaka rais Alassane Ouattara, kutangaza msamaha kwa mume wake kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba.

Kiongozi wa chama cha FPI Simone Gbagbo amefanya mkutano na waandishi wa habari Agosti 11, 2020 ili kumuunga mkono mumewe aliyekwama nchini Ubelgiji na ambaye ahayumo kwenye orodha za wagombea urais.
Kiongozi wa chama cha FPI Simone Gbagbo amefanya mkutano na waandishi wa habari Agosti 11, 2020 ili kumuunga mkono mumewe aliyekwama nchini Ubelgiji na ambaye ahayumo kwenye orodha za wagombea urais. SIA KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Simone na mumewe walishtakiwa na serikali ya rais Ouattara, kutokana na mauaji ya baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya Elfu tatu.

Aliachiliwa kwa msamaha mwaka uliopita huku mumewe ambaye amekuwa katika Mahakama ya Kimatifa ya ICC akiachiliwa huru mwaja uliopita, lakini kwa sasa anaishi nchini Ubelgiji.

Chama cha Gbagbo kimekuwa kikitaka rais huyo wa zamani kuruhusiwa kurejea nyumbani ili kuwania urais.

Hivi karibuni chama cha rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo, FPI kilimtaka rais huyo wa zamani kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Lakini, kuwania kwa Gbagbo, ambaye alikataa kujiuzulu baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2010 kupingwa, na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyogharimu maisha ya watu 3,000 , kunaibua maswali mengi nchini humo, ambapo baadhi wana hofu ya kutokea machafuko mapya.

Uchaguzi wa Oktoba 31 unaonekana kama kipimo kwa utulivu wa nchi.

Laurent Gbagbo aliachiliwa huru mwaka jana na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) katika kesi yake ya uhalifu dhidi ya binadamu na kwa sasa anaishi nchini Ubelgiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.