Pata taarifa kuu
MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Waziri Mkuu wa Mali autaka upinzani kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa

Siku moja baada ya serikali ya mawaziri sita kuundwa nchini Mali, Waziri Mkuu wa Mali Boubou Cissé ametolea wito upinzani kushiriki katika mazungumzo kwa minajili ya kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Waziri Mkuu wa Mali Boubou Cissé, hapa ilikuwa mwezi Machi 2020 huko Bamako.
Waziri Mkuu wa Mali Boubou Cissé, hapa ilikuwa mwezi Machi 2020 huko Bamako. MICHELE CATTANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa serikali mpya yenye mawaziri sita walikutana Jumanne wiki hii katika ofisi ya waziri mkuu, kwa mujibu wa mwandishi wetu huko Bamako, Serge Daniel. Mbele ya waandishi wa habari, Waziri Mkuu wa Mali amezungumzia malengo ya timu yake. "Lengo kuu la serikali hii ndogo ni kuweza kujadili kwa muda muafaka kuhusu jinsi gani Mali inaweza kuondokana na mgogoro huu", amesema Boubou Cissé.

Timu bado haijakamilika na itakamilika hivi karibuni, ameongeza Waziri Mkuu. Boubou Cissé anataka upinzani kushiriki katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Keita ambaye tangu mwezi Aprili amekuwa hana baraza la mawaziri, ameliunda baraza hilo chini ya shinikizo la Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ambayo imehusika katika juhudi za kutanzua mzozo wa nchi yake.

Mawaziri watatu wamerejea katika nyadhifa zao za awali, ambao ni Waziri wa Ulinzi Ibrahima Dahirou Dembele, Waziri wa Utawala wa Kimajimbo Boubacar Alpha Bah na Waziri wa Mambo ya Kigeni Tiebile Drame.

Wapya walioingia ni Kassoum Tapo aliyeteuliwa kuwa waziri wa sheria, Abdoulaye Daffe aliyewekwa katika wizara ya fedha, na Bemba Moussa Keita ambaye amekabidhiwa wizara ya usalama wa ndani.

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi, ECOWAS, linalitaka bunge la Mali kujiuzulu na kuruhusu kuitishwa uchaguzi mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.