Pata taarifa kuu
UNSC-ETHIOPIA-MISRI-SUDAN-USHIRIKIANO

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili mzozo kati ya Ethiopia, Misri na Sudan

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatahmini pendekezo la Misri na Sudan kuhusu mzozo unaozihusisha na Ethiopia baada ya Ethiopia kutaka kujaza bwawa lake la umeme kwenye mto wa Blue Nile.

Bwawa kubwa la Grande Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Blue Nile. picha iliyopigwa Machi 2015.
Bwawa kubwa la Grande Renaissance lililojengwa nchini Ethiopia katika mkoa wa Benishangul Gumuz, kwenye Mto Blue Nile. picha iliyopigwa Machi 2015. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho kinafanyika wakati katikati mwa wiki hii iliyopita nchi hizo tatu (Ethiopia, Misri na Sudan) zilikubaliana kwamba Ethiopia itachelewesha kujaza bwawa lake la umeme kwenye mto wa Blue Nile na kufanya mazungumzo kumaliza mzozo. Hatua hii imekuja baada ya wiki kadhaa za malumbano na vitisho.

Awali Ethiopia ilikuwa imeamua kuanza kujaza bwawa lake la mabilioni ya dola la Grand Renaissance mnamo mwezi Julai.

Misri na Sudan zote zililiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita kuingilia kati mzozo huo uliodumu kwa miongo kadhaa.

Ethiopia imekuwa ikipaza sauti kuhusu nia yake ya kujaza bwala hilo, ambalo inasema ni muhimu kwa mahitaji yake ya umeme na maendeleo. Inasema mradi huo wa bwawa la umeme wenye thamani ya dola bilioni nne, utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 6,450 na utasidia kuwaondoa mamilioni ya watu kutoka kwenye dimbwi la umaskini.

Misri kwa upande mwingine, inautegemea mto Nile kwa asilimia 97 ya mahitaji yake ya maji safi. Inasema bwana hilo linaweza kupunguza ugavi wake wa maji na kuwa athari mbaya kwa wakaazi wake. Sudan pia inategemea mto Nile kwa ugavi wa maji na imetoa mchango muhimu katika kuzileta pande mbili pamoja.

Misri na Ethiopia zote zilikuwa zimetoa uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi kulinda maslahi yao, na kuibua hofu ya kutokea kwa mgogoro wa wazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.