Pata taarifa kuu
DRC-AJIRA-UCHUMI-USALAMA

Serikali ya DRC kuongeza zaidi ya ajira kwa kipindi cha miaka mitano

Waziri wa Viwanda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Julien Paluku amesema serikali ya nchi hiyo kupitia wizara yake imejipanga kuongeza zaidi ya ajira Milioni moja katika kipindi cha miaka Mitano.

Eneo la kibiashara katika Wilaya ay Gpmbe mjini Kinshasa, mji mkuu waDRC, Aprili 19, 2020.
Eneo la kibiashara katika Wilaya ay Gpmbe mjini Kinshasa, mji mkuu waDRC, Aprili 19, 2020. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa juma lililopita jijini Kinshasa, Waziri wa Viwanda nchini DRC Julien Paluku Kahongya amefahamisha kuwa nchi hiyo imebuni mpango mpya wa kitaifa unaolenga kukuza viwanda na hivyo kufanikisha upatikanaji wa kazi zenye tija nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Julien Paluku, amesema mpango uliowasilishwa wakati wa kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi, Juni 5 uliidhinishwa kwa kauli moja, ili kuhakikisha ajira milioni moja zinapatikana ndani ya kipindi cha miaka 5.

Wizara ya Viwanda nchini DRC imeendelea kuimarisha na kufufua baadhi ya viwanda ambavyo tangu miaka ya sitini vilisimama na kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika taifa hilo kubwa na lenye utajiri wa mali asili ambalo limekwamishwa na historia ya uporaji, unyonyaji, na sasa raia wake ni miongoni mwa maskini zaidi barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.