Pata taarifa kuu
LIBYA-SYRIA-URUSI-UTURUKI-USALAMA

Utawala wa Syria na waasi sasa wakabiliana, pia, nchini Libya

Ikiwa vita kati ya serikali na waasi vimepoteza nguvu nchini Syria baada ya Urusi na Uturuki kuzitaka pande hasimu kusitisha mapigano, sasa mzozo huo umehamia nchiniLibya, ambapo mamluki kutoka kambi zote mbili (Urusi na Uturuki) wanakabiliana.

Mmoja wa askari wa kundi la (LNA) linaloongozwa na Khalifa Haftar akielekeza silaha yake kwenye picha ya rais wa Uturuki Tayyip Erdogan iliyobandikwa kwenye gari lla kijeshi la jeshi la Uturuki, ambalo ANL ilitangaza kuwa imelidhibiti baada ya mapigano.
Mmoja wa askari wa kundi la (LNA) linaloongozwa na Khalifa Haftar akielekeza silaha yake kwenye picha ya rais wa Uturuki Tayyip Erdogan iliyobandikwa kwenye gari lla kijeshi la jeshi la Uturuki, ambalo ANL ilitangaza kuwa imelidhibiti baada ya mapigano. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Ankara inasaidia makundi ya waasi nchini Syria na Serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa nchini Libya.

Kwa upande mwingine Moscow inasaidia kijeshi serikali ya Syria ya Bashar al-Assad na inasaidia kwa zaidi ya mwaka mmoja wa vikosi vya Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita huko mashariki mwa Libya, ambaye analenga kudhibiti mji mkuu wa Tripoli, makao makuu ya serikali ya umoja (GNA).

Mzozo wa hivi karibuni kati ya Damascus na Marshal Haftar ulionyesha kuongezeka kwa mizozo hii miwili.

Mapema mwezi Machi, serikali ya mashariki mlwa Libya inayoungwa mkono na Marshal Khalifa Haftar ilifungua tena ubalozi wa Libya katika mji mkuu wa Syria, ubalozi ambao ulikuwa ulifungwa tangu mwaka 2012. Pia zimeanzishwa safari za ndege kutoka Damascus kwenda Benghazi, ngome kuu ya Khalifa Haftar, kilomita 1,000 kutoka Tripoli.

Kulingana na ripoti ya siri ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa, ndege hizo za kampuni ya kibinafsi ya Syria Cham Wings zimewezesha mamia ya mamluki kwenda kwenye uwanja wa vita nchini Libya.

Kulingana na ripoti hii ya wataalam wanaosimamia vikwazo vya silaha vilivyowekwa dhidi Libya, ndege hizo zimefanya safari 33 tangu Januari 1 mwaka huu.

"Kulingana na vyanzo kutoka uwanja wa vita, idadi ya wapiganaji wa kigeni kutoka Syria wanaosaidia majeshi ya Marshal Haftar ni 2,000," imebaini nakala hiyo.

Kundi la wataalam wanabaini kwamba wana uthibitisho kwamba baadhi ya wapiganaji hao walisafirishwa na ndge za shirika la ndege la Cham Wings, kwa "mkataba" wa miezi mitatu.

Kulingana na chanzo hicho, wapiganaji hao waliajiriwa na kampuni ya kibinafsi ya mamluki ya Wagner kutoka Urusi kwa niaba ya Marshal Haftar.

Moscow imeendelea kukanusha kuwepo kwa mamluki kutoka nchi hiyo nchini Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.